• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Shigela atoa miezi sita kukamilisha ujenzi wa Jengo la utawala Mlimba

Posted on: June 16th, 2022

RC Shigela aagiza ujenzi jengo la Utawala Mlimba ukamilike Disemba 2022

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Mlimba Wilaya ya Kilombero Mkoani humo, kukamilisha ujenzi wa jengo la Utawala wa Halmashauri hiyo kabla au ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

Jengo la Utawala Halmashauri ya Mlimba

Mkuu huyo wa Mkoa ametoa agizo hilo Juni 16 mwaka huu alipotembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo ukiwemo mradi huo  wa jengo la Utawala ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi wa Wilaya zote aliyoianza Juni 12 mwaka huu.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akikagua ujenzi wa jengo la Utawala

Shigela amesema kwa sasa changamoto ya uwepo wa mvua iliyokuwepo siku za nyuma imekwisha hivyo mkandarasi anatakiwa kufanya kazi yake usiku na mchana na uongozi wa halmashauri ukisimamiwa na wahe. Madiwani uhakikishe ujenzi huo unakamilika ifikapo mwezi Disemba mwaka huu.

“Kile kisingizio cha mvua sasa imekwishakatika, hakikisheni mnakamilisha mradi huu kwa wakati” ameagiza Martine Shigela.

“tunataka ifikapo Disemba mwaka huu tulionao watu wote na wafanyakazi waweze kuhamia hapa na huduma zote ziweze kutolewa hapa “….amesisitiza Shigela.

RC Shigela (kulia mwenye kofia ya bluu) akitoa maagizo ya kukamilisha ujenzi huo. Kulia mwenye kofia nyeupe ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja

Katika hatua nyingine Shigela ameagiza eneo ambapo jengo hilo linajengwa kulifanya kuwa eneo la taasisi za kiserikali zikiwemo Mahakama Kituo cha Polisi, TARURA, Magereza Ofisi ya DC, pamoja na Ofisi za vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama lengo ni kumrahisishia mwananchi kupata huduma za kijamii  kiurahisi zaidi.

licha ya kutembelea ujenzi wa jengo la utawala Mhe. Shigela pia alitembelea ukamilisha wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya

Sambamba na maagizo hayo Mkuu wa Mkoa Martine Shigela ameonekana kufurahishwa sana na mabadiliko na utendaji kazi mzuri wa Halmashauri hiyo ya Mlimba kwa kufanya kazi zake kwa ufanisi na kwa mipango madhubuti lakini pia kwa kutekeleza KWA WAKATI maagizo kemkem ya Serikali.

Kwa sababu hiyo, Shigela amewapongeza Madiwani wote wa Halmashauri hiyo akiwemo Mhe. Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Kamati yake Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo akiongoza wataalamu wake wote kwa kuonesha ushirikiano wanao kwenda nao.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hanji Godigodi amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa pesa Jumla ya shilingi 2.8 Bil. Kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo la utawala pekee huku akiahidi kuendelea kusimamia matumizi ya fedha hizo ili yaendane na uhalisia wa kazi (Value for Money).

baadhi ya majengo ya Hospitali ya Wilaya 

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Innocent Mwangasa.yeye amebainisha kuwa hawana mgogoro wowote na Mkandarasi anatekeleza mradi huo katika kutekeleza majuskumu yake na kwamba anafanya kazi yake kikamilifu huku akimtaka aendelee na uzalendo huo kwa maslahi mapana ya Watanzania.

Mkuu wa Mkoa Martine Shigela pamoja na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa hospitali hiyo ambayo tayari imeshaanza kutoa huduma kwa wagonjwa


Mradi wa Ujenzi wa Jengo la utawala una gharama ya jumla ya shilingi 2.8 ambazo zimetolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Suluhu Hassan na ulinaza Juni 2021 na ulitakiwa kukamilika mwezi Juni 30 mwaka huu na umechelewa kukamilika kwa sababu ya changamoto ya mvua na sasa mkandarasi anatakiwa kukamilisha kazi hiyo Disemba mwaka huu.

akiongea na watumishi

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhe. Innocent Mwangasa (kushoto)


MWISHO

 

.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.