Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amewaagiza Viongozi Mkoani humo kukamilisha ujenzi wa majengo ya UVIKO – 19 kabla au ifikapo Juni 30 mwaka huu kwa kufanya kazi hiyo usiku na mchana na kuongeza wataalamu wakiwemo wakandarasi na mafundi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akikagua jengo la huduma ya dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero wakati ziara yake Wilayani humo, kushoto mwa Mkuu wa Mkoa ni Mkuu wa Wilaya hiyo Bi. Halima Okash.
RC Morogoro (mwenye shati la maua) akipokelewa na baadhi ya wahandisi ali[potembelea site ya ujenzi wa wa Jengo la Dharura
Martine Shigela ametoa kauli hiyo hivi karibuni wakati wa ziara yake ya siku moja Wilayani Mvomero alipotembelea ujenzi wa miradi ya maendeleo na kutatua kero za wananchi ambapo alikagua Ujenzi wa Jengo la Dharura katika Hospitali ya Wilaya hiyo, lenye thamani ya shilingi 300 Mil. zilizotolewa na Serikali.
Amesema, Majengo hayo ya kimkakati ambayo fedha zake zinatokana na program ya UVIKO - 19 hazitakiwi kuvuka mwaka huu wa fedha 2021/2022 lakini pia malengo ya fedha hizo zilizokopwa kutoka shirika la fedha Duniani – IMF yaweze kutimia na serikali kuaminiwa hivyo kuweza kupewa mkopo mwingine wa masharti nafuu kwa maendeleo ya wananchi wake.
Kwa sababu hiyo, Mkuu wa MKoa Martine Shigela ametoa maelekezo ya kufanya kazi ya ujenzi wa miradi hiyo usiku na mchana na kuongeza wafanyakazi ili kukamilisha ujenzi wa majengo kwa muda uliopangwa.
“kwa hiyo hakikisheni kama ambavyo nimeeleza hapa, ujenzi ufanyike usiku na mchana…lakini kama kuna mahala ambapo mnaweza kuongeza wataalamu hakikisheni mnaongeza wataalamu hasa wajenzi, wakandarasi na mafundi…” ameelekeza Shigela.
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan imetoa jumla ya Shilingi 690,000,000.00 kwa ajili ya kuongeza baadhi ya majengo muhim ya Hospitali ya Wilaya ya Mvomero ambayo iko Km.1.5 kutoka Barabara kuu ya Dodoma – Morogoro likiwemo Jengo la Dharura, nyumba ya watumishi (3 in One), wodi ya wanawake, kichomea taka na njia za kutembelea wagonjwa katika Hospita hiyo.
Muonekano wa jengo la dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.