• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Simbachawene ataka shughuli za Nanenane kuwa endelevu

Posted on: August 8th, 2022

SIMBACHAWENE AAGIZA SHUGHULI ZINAZOFANYIKA NANENANE KUWA ENDELEVU

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge George Simbachawene ameagiza shughuli za maonesho zinazofanyika viwanja vya nanenane ziwe endelevu kwa mwaka mzima ili kufanya eneo hilo kuwa kitovu cha teknolojia katika sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi.

Waziri Simbachawene ametoa agizo hilo leo Agosti 8 mwaka huu wakati akifunga maonesho ya Wakulima maarufu kama nanenane Kanda ya Mashariki yaliyofanyika katika viwanja vya mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyopo Nanenane  Katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais  wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla kwenye maonesho hayo ya nanenane kanda ya mashariki yanayoshirikisha mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro, Waziri Simbachawene ametoa wito wa kusambaza kwa wananchi teknolojia mpya za kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kukuza uchumi wao huku akitaka akitaka shughuli hizo kuwa endelevu kwa mwaka mzima

Katika hatua nyingine Waziri Simbachawene amewataka Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Mikoa hiyo minne kutekeleza Maagizo ya viongozi wote waliotembelea maonesho ya mwaka huu waliyoyatoa wakati wakitembelea maonesho hayo.

Mwisho, Waziri George Simbachawene ameagiza maonesho hayo ya nanenane yatumike kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Kilimo Anthon Mavunde ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza Bajeti ya Wizara ya Kilimo kutoka shilingi Bil. 294 kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 hadi shilingi Bil. 954 kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Aidha, amesema Wizara hiyo ipo kwenye mipango ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji na tayari wameanza kuyapitia mabonde makubwa 22 hapa nchini yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na kuyafanyia utafiti ili kujenga miradi mikubwa ya umwagiliaji


Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amejikita akiongea katika hafla hiyo amesema Mkoa umejipanga kukomesha changamoto kubwa inayoukabili Mkoa wa Morogoro ambayo ni Migogoro ya Wakulima na Wafugaji na kwamba wanajipanga kutenganisha maeneo ya wakulima na wafugaji ili kukomesha migogoro hiyo.

Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amesema maonesho ya Nanenane ya mwaka huu pamoja na kuwa yamechelewa kuanza amebainisha kuwa takribani wananchi 70,000 kutoka sekta za Kilimo, Mifugo na Uvuvi wametembelea maonesho hayo.

Maonesho ya Nanenane ya mwaka huu yaliyokuwa na kaulimbiu ya ajenda ya kumi ya thelathini, Kilimo ni Biashara, shiriki kuhesabiwa kwa mipango Bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi yamehitimishwa rasmi leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Uratibu na Bunge Mhe. George Simbachawene

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.