Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa anawatangazia wadau wote wa NISHATI Mkoani Morogoro kushiriki mjadala wa kitaifa wa “NISHATI SAFI YA KUPIKIA” ulioandaliwa na Wizara ya Nishati utakaofanyika kuanzia Novemba 1 – 2, 2022 katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Mjadala unalenga kuweka mikakati ya namna ya upatikanaji wa nishati safi ya kupikia.
Washiriki mbalimbali kutoka Serikalini, Sekta binafsi, Asasi za kiraia na wadau wengine wanatarajia kushiriki mjadala huo, Mgeni rasmi atakuwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkoa wa Morogoro ni mojawapo ya kituo kitakachoshiriki mjadala huo mubashara. Kimkoa mjadala huu utafanyika Morena Hotel ghorofa ya Pili.
Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Morogoro, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri, Viongozi kutoka SUA, TAWA, TFS, BONDE LA WAMI RUVU na TANAPA mnaombwa kushiriki bila kukosa.
Waalikwa wengine ni pamoja na NEMC, TANESCO, MKAA ENDELEVU, Kiwanda cha Rice Millers Kihonda, Viongozi wa Kikundi cha Majiko Banifu, na wadau wengine pia mmealikwa.
Tangazo hili limeandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.