TANROADS Morogoro yaongezewa bajeti
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutoa fedha katika Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matengenezo ya barabara na miundombinu mingine na kuongezeka kutoka Tsh. Bil. 24.8 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Tsh. Bil. 26.02 mwaka 2021/2022.
Katibu Tawala wa Mkoa wa morogoro Mariam Mtunguja akitoa maneno ya utangulizi kabla ya Mkuu wa Mkoa hajafungua kikao hicho
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela wakati akifungua kikao cha 37 cha Board ya Barabara Mkoa wa Morogoro kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ualimu Morogoro leo Oktoba 7, 2021.
RC Morogoro Martine Shigela akifungua kikao cha 37 cha Road Board
Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa kwa upande wa Bajeti ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ilikuwa Tsh. Bil. 2.75 na kuongezeka hadi Tsh. Bil. 5.37 mwaka 2021/2022 zikiwemo Tsh. Bil. 2.4 iliyotolewa kwa ajili ya Barabara ya Bigwa – Kiloka Km. 15 kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la kilosa akitoa mchango wake wa mawazo kwenye kikao cha Road Board Mkoani Morogoro
Baadhi ya Wahe. Wabunge wa Mkoa wa Morogoro wakichangia hoja kwenye kikao hicho
Aidha imeelezwa kuwa Bajeti ya matengenezo ya barabara za vijijini na Mijini chini ya Wakala wa Barabara TARURA katika mwaka wa fedha 2020/2021ilikuwa shilingi Bil. 8.07 na mwaka huu 2021/2022 bajeti imeongezeka kufikia Tsh. Bil 8.23.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Morogoro wakichangia hoja
Kwenye bajeti ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 chini ya TARURA ilitengwa bajeti ya Tsh. Mil. 400 na mwaka 2021/2022 bajeti imeongezeka hadi kufikia Bil. 23.93.
Wakijadili sekta hiyo ya Miundombinu ya Barabara Wajumbe walio wengi wa kikao hicho walionekana kufurahishwa na utendaji kazi wa TANROADS na TARURA Mkoani humo huku wakiwataka watendaji hao kuongeza juhudi kiutendaji badala ya kubweteka na pongezi zilizotolewa kwao na wajumbe wa kikao hicho .
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.