TARURA YATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MOROGORO
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetoa mafunzo kwa waandishi wa Habari juu ya ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maegesho ya vyombo vya moto vya usafiri wa nchi kavu kwa kutumia mfumo mpya wa kielektroniki ambao kwa Mkoa wa Morogoro unagtarajiwa kutumika kuanzania Mwezi Machi Mosi mwaka huu.
Kikao hicho ambacho kimefanyika Februari 22 mwaka huu katika ukumbi wa Ofisi za TARURA Mkoa uliopo mkabala na standi ya zamani ya mabasi madogo (Hice) ya Mjini Morogoro katika Halmashauri ya Manispaa Morogoro kimelenga zaidi kuwaelimisha waandishi wa habari juu ya kanuni na taratibu zitakazotumika mara utaratibu huo mpya utakapoanza.
Akiongea na waandishi wa habari kwa niaba ya Mwanasheria TARURA Bw. Shaban Mdagano, Bi. Tausi Madebo ambaye pia ni mwanasheria Mkoa wa Morogoro amesema ameeleza umuhim wa Waandishi wa Habari kuzijua baadhi ya kanuni zinazoendana na mfumo huo ili waweze kuuelimisha umma na kuzifuata kikamilifu.
Bi Tausi amezitaja baadhi ya kanuni zinazotakiwa waandishi wa Habari na wananchi kuzijua ni pamoja na Mteja kutakiwa kulipa ushuru wa maegesho aliyofanya ndani ya siku 14. Mteja anayeshindwa/anayekataa kulipa USHURU huo wa maegesho kwa kipindi hicho atatakiwa kulipa faini ya shilingi 10,000/= pamoja na ushuru wa maegesho aliotakiwa kulipa.
Ameendelea kufafanua kuwa Mteja huyo endapo atashindwa kulipa faini hiyo, lakini akakubali kosa lake atatakiwa kujaza fomu maalum ya kufifilisha kosa hilo na kutakiwa kulipa faini ya shilingi 30,000/= na endapo hatokubali kosa hilo na kujaza fomu hiyo atatakiwa kufikishwa mahakamani ambako huko akithibitika ana kosa atalazimika kulipa fani ya shilingi 300,000/= au kifungo cha miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja.
Hadi Sasa mfumo huu umeanza kutumika katika Mikoa mitano hapa nchini ambayo ni pamoja na Mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma, na Mkoa wa Dar es Salaam.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.