Mhandisi Ezron Kilamhama Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundo mbinu akiwa kwenye kikao cha Tume ya Haki Jinai
Balozi Ombeni Sefue ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai akiwasikiliza wajumbe mbalimbali wa Tume ya Haki jinai (Hawapo pichani) leo hii katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Tume ya kuangalia namna ya kuboresha taasisi za haki jinai iliyoundwa na Rais Mhe. DKT. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni imewasili Mkoani Morogoro kwa ziara ya kukusanya maoni kwa wananchi wa Mkoa wa Mororgoro.
Zoezi la ukusanyaji wa maoni na mapendekezo kutoka kwa wadau mbalimbali ikiwa pamoja na viongozi wa dini kwenye kikao.
Akithibitisha ziara hiyo Balozi Ombeni Sefue ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo leo Machi 9, 2023 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, amesema ziara hiyo inahusu ukusanyaji wa maoni na mapendekezo ili kuboresha taasisi za haki jinai.
Akifafanua zaidi Balozi Ombeni Sefue amesema tume hii imegawanyika katika Mikoa mbalimbali ukiwemo mkoa huu wa Morogoro ambapo sisi tupo ili kupata tathmini ya Mkoa kuhusu haki jinai kwa kukusanya maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro...”
Aidha, amebainisha lengo la ziara hiyo Mkoani humo kuwa ni kupokea tathmini juu ya tume hiyo na kukusanya maoni, changamoto, mapendekezo na ushauri kutoka kwa wadau mbalimbali na wananchi kuhusu mfumo huo lengo ni kuuboresha.
Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akiwa katika picha na viongozi mbalimbali kweye kikao cha Tume ya Haki Jinai mkoani Morogoro.
Sambamba na hayo Balozi Ombeni Sefue aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi hapa nchini amesema tume yake imepokea mapendekezo mengi yanayoboresha Taasisi za haki Jinai ikiwa ni pamoja na kuwa na mfumo haki jinai unaoleta maridhiano na kufuata yale yote dini zetu zinazotufundisha kwani haki ni muhimu zaidi.
Viongozi wa Dini wakichangia mapendekezo na maoni kwenye kikao cha Tume ya Haki Jinai Mkoani Morogoro
Hata hivyo, Tume hiyo imekutana na viongozi wa dini ambao wametoa maoni na mapendekezo kwa ajili ya kulinda Amani ya nchini
Ilikukamilisha azima hiyo tume pamoja na kuazimia kukutana na wadau mbalimbali mkoani humo, kwanza imekutana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Morogoro na kupokea maoni juu ya kuboresha taasisi za Haki jinai
Alex Mukama kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro akiwa katika kikao cha Tume ya haki Jinai
MWISHO.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.