Serikali inaendelea na juhudi za kupunguza kama sio kuondoa kabisa migogoro ya Ardhi hapa nchini hususan Mikoa yenye changamoto za migogoro ya Ardhi ukiwemo Mkoa wa Morogoro.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa (Aliye vaa koti la Bluu bahari) akiwa kwenye picha ya pamoja na Timu ya Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi kutoka Dodoma ambayo imekuja kuandaa mipango ya matumizi bora ya Ardhi Wilayani Ulanga. Kutoka kulia ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu Mhandisi Ezron Kilamhama.
Leo Oktoba 30, Tume ya Matumizi Bora ya Ardhi kutoka Dodoma kwa kushirikiana na Frank Zoological Society na TANAPA imefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kujitambulisha na kusaini kitabu ili kwenda Wilaya ya Ulanga kuandaa mipango ya matumizi bora ya Ardhi.
Tume hiyo imepewa jukumu la kuandaa mipango ya matumizi Bora ya Ardhi katika Vijiji 5 ambavyo ni Chilombora, Euga, Gombe, Nkongo na Mzelezi katika Wilaya ya Ulanga.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.