• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

TUME YA UCHAGUZI YAWATAKA WANANCHI KUJITOKEZA KUBORESHA TAARIFA ZAO.

Posted on: February 18th, 2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele ametoa rai ya kuwataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la mpiga kura ifikapo Machi Mosi, 2025 kwani amesema hiyo ndio njia pekee ya kushiriki uchaguzi mkuu ujao wa Rais, wabunge na madiwani utakaofanyika mwezi Novemba mwaka huu.


Mwenyekiti Mwambegele ametoa rai hiyo Februari 18, mwaka huu wakati akifungua mafunzo ya siku 2 kwa watendaji ngazi ya Wilaya kuhusu uboreshaji wa daftari la mpiga kura yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Magadu iliyopo Manispaa ya Morogoro yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo watendaji hao kwa kutumia mfumo wa kisasa ujulikanao kama Votes Regislation System (VRS).


Aidha, Jaji Mwambegele amewataka watendaji hao kushirikiana  na wataalam wengine wa Serikali waliopo katika maeneo yao pamoja na wananchi katika kutoa Elimu ya kutumia mfumo huo wa kisasa  ili kufanikisha kwa ufanisi zoezi la uboreshaji taarifa zao ili kushiriki uchaguzi huo mkuu.


Sambamba na hayo, Jaji Rufaa Jacobs amesema kuwa wakati wa uboreshaji wa daftari hilo la kudumu, mawakala wa vyama vya siasa watapata nafasi ya kuwepo kwenye vituo vya uandikishaji huku akiwataka kutoingilia kazi za watendaji wa vituo vya kujiandikishia wapiga kura kwenye vituo watakavyopangiwa.


”….wakati wa uboreshaji wa daftari, mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo kwenye vituo vya kujiandikishia wapiga kura jambo hili ni muhimu kwani litasaidia kuleta uwazi katika zoezi nzima" amesema Jaji Mwambegele.


...lakini pia mawakala hao watasaidia kutambua waombaji wa eneo husika hivyo kupunguza kutotokea vurugu zisizo za lazima". Ameongeza.


Sambamba na ushauri huo Jaji Mwambegele amesema tume imetoa vibali kwa asasi za kiraia 157 kwa ajili ya kutoa elimu ya mpiga kura pia imetoa kibali kwa taasisi na asasi za kiraia 42 kuwa waangalizi  watakao shiriki katika zoezi zima la uandikishaji, taasisi 9 kati ya hizo ni za kimataifa na 33 ni kutoka ndani ya nchi.


Kwa upande wake, Afisa muandikishaji wa Jimbo la Morogoro Mjini Bw. Faraja Madugu, amesema zoezi hilo ni la muhimu kwani ndio kitovu cha ufanisi wa zoezi zima ambapo wapiga kura watapata fursa ya kuchagua viongozi wanaoona wanawafaa katika kuwaletea maendeleo.


Zoezi la uandikishaji ambalo kitaifa lilifunguliwa Mkoani Kigoma linakwenda na kaulimbiu isemayo “kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa uchaguzi bora”


Mwisho.


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.