Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameahidi kuendelea kujenga miundombinu ya barabra itakayounganisha Mkoa wa Morogoro na Mikoa ya Njombe na Iringa kwa lengo la kuwezesha usafiri na usafirishaji wa mazao ya chakula na bishara kutoka katika mikoa hiyona na kufanya hiyo kufunguka kiuchumi.
Dkt. Samia amesema hayo Agosti 4, 2024 wakati wa uzinduzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara yenye urefu wa kilometa takribani 67 pamoja na daraja la mto Ruaha lililopo Wilayani Kilombero ambapo limegharimu zaidi ya shilingi Bilioni 157 hadi kukamilika kwake ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya siku 6 Mkoani Morogoro.
Dkt Samia Suluhu Hassan amesema kukamilika kwa ujenzi wa Daraja na barabara hiyo ni moja ya hatua ya kuanza kuunganisha Mkoa wa Morogoro na mikoa ya Njombe na Ruvuma huku akibainisha kuwa Serikali itahakikisha maeneo hayo wanajenga miundombinu ya kutosha kwa sababu ya uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula uliopo unaopeleka chachu ya maendeleo katika Mikoa hiyo na Tanzania Kwa ujumla.
".. Ni ahadi ya Serikali Kwamba tunakwenda kuijenga njia hiyo mpaka tuweze kuunganisha Mkoa wa Morogoro na Mikoa mingine inayopakana nayo.." amesema Dkt. Samia
Dkt. Samia amesema moja ya lengo la ziara yake katika Mkoa wa Morogoro pamoja na kuangalia miradi ya maendeleo pia ni kuangalia adhari za mvua kubwa zilizonyesha mwaka huu na kutoa maagizo kwa wizara ya ujenzi kufanyia marekebisho ya miundombinu ya barabara iliyoharibiwa kuwa mizuri ili kurahisisha usafiri na usafirishaji.
Katika ziara hiyo pia Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanda cha Sukari cha Kilombero ambapo ujenzi huo unaendelea vizuri mbao hadi sasa umefikia asilimia 83 na unatarajiwa kukamilika mwezi wa Juni 2025.
Imeelezwa kuwa kiwanda hicho kitakapokamilika kitaongeza uzalishaji wa bidhaa ya sukari nchini na kufanya utoshelevu wa bidhaa hiyo kwa watumiaji, pia kitasaidia kutunza fedha za kigeni kwa kuacha kuagiza bidhaa hiyo nje ya nchi.
MWISHO.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.