• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Uboreshaji wa daftari la kudumu kuanza rasmi Machi mosi Morogoro

Posted on: February 17th, 2025

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele amesema uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utaanza kufanyika rasmi Machi 01 had 07, Mwaka huu Mkoani Morogoro. ili kupata fursa ya kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika Novemba, 2025.


Jaji Mwambegele amethibitisha hayo Februari 17, Mwaka huu katika Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya magadu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.


Aidha, Mwenyekiti huyo amesema Tume hiyo imeanza maandalizi wa uboreshaji wa daftari la mpiga kura ambapo itahusisha matumizi ya mifumo ya kielektroniki (BVR) ili kurahisisha uboreshaji huo na kuhifadhiwa kwenye kanzidata ya wapiga kura.


“Kwa mujibu wa ratiba, kwa sasa Tume imeanza maandalizi ya mzunguko wa 12 kati ya mizunguko 13 ya uboreshaji wa Daftari. Mzunguko huu wa 12 unahusisha Mkoa huu wa Morogoro” amesema Jaji Mwambegele.


Vilevile, Jaji huyo amesema Tume hiyo imekamilisha zoezi hilo katika Mikoa 27 ikiwemo Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma na Singida. Mikoa mingine ni Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe, Ruvuma, Lindi na Mtwara.


Kwa sababu hiyo, Jaji Jacobs amewasisitiza wadau mbalimbali kuhamasisha wananchi na kutoa elimu ili kujitokeza kwa wingi kujiandikisha,  kurekebisha na kuboresha taarifa zao huku akiwataka wazee, watu wenye walemavu, wagonjwa, wajawazito na wakina mama wenye watoto wachanga watapewa kipaumbele.


Kwa upnde wake, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC, Bw. Kailima Ramadhani amesema Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 302,752 Mkoani Morogoro sawa na ongezeko la asilimia 18.7 ya wapiga kura 1,612,952 waliokuwepo kwenye daftari la wapiga kura mwaka 2020.


Naye, Balozi Omar Mapuri ambaye ni Mjumbe wa Tume hiyo amesema Tume itazingatia usimamizi wa katiba, sheria na kanuni za uchaguzi katika zoezi hilo muhimu kwa mustakabali wa Taifa la Tanzania huku akiwataka wadau wa uchaguzi  kushirikiana na wananchi kwa kuwapa elimu ya uboreshaji taarifa zao.


Zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura ambapo uzinduzi wake ulifanyika Mkoani Kigoma Julai 20, Mwaka huu lenye kaulimbiu isemayo "Kujiandikisha kuwa Mpiga Kura ni Msingi wa Uchaguzi Bora".


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.