Ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro inayojengwa pembezoni mwa Ofisi ya sasa ya Mkuu wa Mkoa huo unaendelea kwa kasi kama ilivyotarajiwa na Mkandarasi wa ujenzi huo alivyoahidi.
Muonekano wa jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa litakapo kamilika 2024.
akizungumza na mwandishi wa HABARI hii, Mkandarasi wa jengo hili Mhandisi Queen Sanga amemhakikishia mwandishi kuwa jengo hilo litakamilika kwa wakati kama alivyoahidi wakati anakabidhiwa kazi hiyo na kwamba watafanya kazi usiku na mchana ili wakamilishe kwa wakati.
Muonekano wa majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro yanayotumika kwa sasa.
Ujenzi wa jengo hilo lenye zaidi ya ghorofa mbili utagharimu zaidi ya Tsh. Bilioni 6 na tayari Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekwisha peleka fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi huo wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya picha za jengo jipya la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa likiendelea kujengwa.
kwa Mujibu wa mkataba ujenzi wa jengo la Ofisi Mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ni wa kipindi cha miaka miwili (2) kuanzia 27 Mei hadi 26 Mei 2024.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.