• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

Posted on: June 11th, 2025



Kikao cha Baraza Maalum la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kimeibua hoja ya upungufu wa watumishi wa Serikali wa sekta ya Elimu na Afya wilayani humo ambapo sekta ya elimu ina upungufu wa walimu 800 kwa shule za msingi na Sekondari sawa na asilimia 41 na Sekta ya Afya ina upungufu wa watumishi zaidi ya 500 sawa na asilimia 70 ya upungufu wa watumishi wote.

Hayo yamebainishwa Juni 10, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, wakati wa kikao Maalum cha baraza la madiwani cha kupitia na kutathmini hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuzipatia majawabu hoja hizo.

Akieleza zaidi Mkuu huyo wa Mkoa amesema changamoto hiyo inakwamisha utoaji bora wa huduma kwa wananchi ambapo baadhi ya shule wilayani humo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa walimu hali inayoathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya wanafunzi na utoaji wa huduma za Afya.

Hivyo ameitaka Menejimenti ya Halmashauri hiyo kuendelea kufuatilia utekelezaji wa mapendekezo ya CAG kwa ukaribu na kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti mapungufu hayo na kuhakikisha huduma kwa wananchi hazikwami kwa kuwa suala la rasilimali watu ni la kipaumbele.

"..menejimenti mkasimamie kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa kujenga hoja ya pamoja ili kupata watumishi hao.." amesema Mhe. Adam Malima.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba Mhe. Innocent Mwangasa amesema Halmashauri hiyo kwa miaka mitano mfululizo  imeweza kupata hati safi hivyo amemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendele kutoa fedha kwa ajili ya maenendeleo ya Halmashauri hiyo.

Aidha, Diwani  wa Kata ya Mbingu Mhe. Nestory Kilula amesema kwenye sekta ya Afya wanaupungufu wa vifaa tiba na wataalamu wa afya jambo linalopelekea wananchi kushindwa kupatiwa huduma mahususi kwa wakati, hivyo amemuomba Mhe. Rais kuongezewa wataalamu wa Afya kwenye vituo vya Afya na zahanati ili waweze kuwahudumia wananchi pasipo na dosari.

Naye Diwani wa Kata ya Kalengakelu Mhe. Martha Daniel amesema upungufu wa walimu katika shule za Msingi na sekondari kunapelekea walimu kuzidiwa na wingi wa wanafunzi jambo linalopelekea wanafunzi kukosa umakini katika kupata elimu hivyo ameiomba Serikali kuhakikisha wanatatua changamoto hiyo.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • HOJA ZA MANUNUZI ZASABABISHA RC KUTOA MAAGIZO MAZITO IFAKARA.

    June 09, 2025
  • WANATUHUMIWA KUUZA MALI ZA USHIRIKA MOROGORO.

    June 07, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.