MFUMO MPYA WA UKUSANYAJI MAPATO YA MAEGESHO YA VYOMBO VYA MOTO KUANZA KUKUSANYWA KIDIJITALI.
Ukusanyaji wa mapato yatokanayo na maegesho ya vyombo vya moto vya usafiri wa nchi kavu Mkoani Morogoro utaanza kukusanywa kwa kutumia mfumo wa kielektroniki kuanzia Machi Mosi mwaka huu, imefahamika.
Taarifa hiyo imetolewa Februari 9, mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Martine Shigela wakati anaongea na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
DC Morogoro Albert Msando akitoa taarifa ya mabadiliko kwa waandishi wa habari kuhusu ukusanyaji ushuru wa maegesho ya vyombo vya moto kuwa wa kidijitari
Albert Msando Amesema makusanyo hayo kwa Sasa yatafanyika kwa kutumia mfumo wa kielektroniki uitwao TerMIS ambapo malipo yote yatafanyika kwa kutumia control namber mfumo ambao Mkoa wa Morogoro ulikuwa haujaanza kuutumia na Sasa unatarajiwa kuanza kutumika rasmi Machi 1, mwaka huu, ameeleza Mkuu huyo wa Wilaya.
Aidha, Mhe. Albert Msando akiongea na waandishi wa habari amebainisha lengo Kuu la mabadiliko hayo kuwa ni pamoja kuongeza mapato ya Serikali, kuepusha matumizi ya fedha mbichi na kuondokana na Kero zilizokuwa zinajitokeza siku za nyuma za kufukuzana na wateja wao.
Kwa sababu hiyo, Mkuu wa Wilaya amewataka watumiaji wote wa vyombo vya moto kufuata utaratibu huo mpya ulioanzishwa na Serikali kupitia Wakala wa Barabara wa Mjini na Vijijini - TARURA wa kulipa ushuru kwa hiari, kwani fedha zinazoparikana zinalenga kusaidia Maendeleo ya wananchi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.
Naye Mkuu wa Kitengo Cha TEHAMA - TARURA Stanley Mlula amesema serikali inahitaji watu kuelewa vema lengo la kutumi contorl number ya GepG ili kuunganisha na namba za vyombo vya usafiri na kuweza kutoa ankara ambayo italipa moja kwa moja kupitia simu au benki ili kurahisisha utendaji kazi katika maeneo yote hapa nchini.
Sambamba na hayo, Mkuu wa Kitengo Cha Sheria - TARURA Shaban Mdagano ameeleza umuhim wa wananchi kuzijua baadhi ya kanuni zinazoendana na mfumo huo ili waweze kutekeleza kwa ufanisi zaidi kanuni hizo.
Baadhi ya kanuni zinazotakiwa kujulikana ni pamoja na Mteja anayeshindwa/anayekataa kulipa USHURU wa maegesho wakati wa kuegesha gari au chombo chake cha moto baada ya Siku Kumi na Nne atatozwa faini ya shilingi elfu kumi pamoja na fedha ulizotakiwa kulipa.
Endapo mteja atashisdwa kulipa tena faini hiyo atafikishwa Mahakamani ambako huko ikithibitika ana kosa mteja atalazimika kulipa faini ya shilingi laki tatu au kifungo cha miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja.
Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja akifungua semina hiyo ya wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na na baadhi ya Viongozi wa Mkoa huu, amesema Mkoa wa Morogoro unaingia katika mfumo wa kukusanya ushuru wa maegesho wa kielektroniki, mfumo huo utaondoa upotevu wa mapato yaliyokuwa hayakusanywi ipasavyo kwani kila mteja atalipa ushuru wa chombo chake anachomiliki kwa kutumia control number.
Hadi sasa Mfumo huu unatumika katika mikoa mitano hapa Nchini mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Mwanza, Singida, Shinyanga, Dodoma na Dar es salaam.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.