Uzinduzi ugawaji miche ya karafuu .
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dk. Mussa Ali Mussa Aprili 18, 2024 amezindua ugawaji miche ya karafuu zaidi ya 10,000 kwa wakulima wa vijiji vya kata tano za Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Ili waweze kupanda ikiwa ni miti rafiki katika utunzaji wa mazingira , vyanzo vya Maji na kuwapatia kipato cha kiuchumi kwa kuuza karafuu ,miche hiyo imenunuliwa na Shirika la WWF kutoka katika vitalu vya vikundi vya wakulima wa Kijiji cha Kibwaya, kata ya Mbuyuni Wilayani humo.
Ikumbukwe kuwa Mkoa wa Morogoro upo kwenye programu ya kulima mazao matano (5) ya kimkakati ambayo ni mazao ya Viungo ikiwemo Karafuu, mdarasini, pilipilimanga, vanila na Iliki. Mazao mengine ni Michikichi, Kokoa, parachichi na Kahawa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.