Mwenyekiti wa Baraza la vyama vya siasa hapa nchini Juma Khatibu amevitaka vyama vya siasa nchini kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa amani na utulivu na kunadi sera za ilani ya vyama hivyo bila fujo jambo ambalo litafanya uchaguzi huo kuwa ws Amani, haki na usawa.
Juma Khatibu ametoa Wito huo Mei 14, 2025 wakati wa kikao cha Baraza la vyama vya siasa ambapo moja ya ajenda ilikuwa ni utoaji wa elimu juu ya masuala ya usawa wa kijinsia kwa vyama vya siasa mada iliyowasilishwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Barani Afrika (WILDAF).
Kiongozi huyo amesema, katika uchaguzi Mkuu wa mwaka huu jumla ya vyama vya siasa 18 vitashiriki huku akitos wito kwa watakaogombea kwenda kusimamia misingi na maadili ya katiba za vyama vyao, kunadi sera za vyama vyao kistarabu na kuweka mbele uzalendo.
".. Sisi viongozi wa vyama vya siasa tushiriki uchaguzi kwa njia ya amani na utulivu na niwaombe twende tukanadi sera ya vyama vyetu vya siasa bila kutoa maneno yasiofaa.." amesisitiza.
Kwa upande wake mtoa mada kutoka WILDAF Bi. Rehema Maro amesema lengo la mafunzo hayo ni kwenda kuboresha mifumo ya kisiasa inayojali haki usawa na uwajibikaji pia ushiriki wa wanawake katika shughuli za kisiasa ndani ya vyama vya siasa na nje.
Naye Katibu Mkuuu wa chama cha National League for Democracy (NLD) Bw. Doyo Hassan Doyo amesema kupitia uundwaji wa madawati ya kijinsia ndani ya vyama vya siasa, yatatokomeza unyanyasaji wa kijinsia ndani ya vyama hivyo na kuwa na usawa wa kijinsia katika nyazifa za uongozi.
Katibu Mkuu wa Chama cha National Convention Contruction and Reform (NCCR- Mageuzi) Bi. Everine Munis amesema kuundwa kwa majukwaa hayo ndani ya vyama vya siasa unalenga wanawake, wanaume, vijana na watu wenye ulemavu katika kuwania nafasi za uongozi na kuwataka wanawake kugombea nafasi mbalimbali ndani ya vyama vyao.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.