WADAU WA KILIMO KANDA YA MASHARIKI WASHAURI KUELEKEA MAONESHO YA NANENANE MWAKA 2022.
Wadau wa kilimo Mkoani Morogoro wameshauri wakulima wenzao, wafugaji na wavuvi juu ya umuhimu wa elimu bora ya kilimo, uvuvi na ufugaji kuelekea sherehe za maonesho ya Nanenane yanayotarajiwa kuanza Agosti na kukamilika Agosti 8 mwaka huu katika viwanja vya MWL. J.K Nyerere Nanenane Mkoani humo.
Akiongea mara baada ya kikao cha wataalamu cha maandalizi ya maadhimisho hayo kilichofanyika jana Agosti 14 mwaka huu Bw. Best Massamba ambaye ni mwakilishi wa tasnia ya Sukari hapa nchini, amesema Msingi mkubwa wa kilimo chenye tija ni wadau wa sekta hiyo kupata elimu bora ya kilimo chenye tija.
Meneja wa Banda la Bodi ya Sukari katika viwanja vya maonesho ya Nanenane ambaye pia ni mwakilishi wa Tasnia ya Sukari hapa nchini Bw. Best Massamba akizungumza wakati wa mahojiano juu ya maandalizi ya Maonesho hayo Julai 14 mwaka huu.
Kwa msingi huo Bw. Massamba amewataka wananchi Mikoa minne inayounda kanda ya Mashariki Tanga, Dar es Salaa, Pwani na wenhyeji Morogoro waweze kujitokeza katika maonesho hayo ili kupata Elimu bora ya Kilimo, Uvuvi na Ufugaji lengo kuu likiwa ni kupata Elimu juu ya kilimo chenye tija ili kuweza kupata mazao bora na hatimaye kumkomboa kiuchumi.
“Wito wangu kwa wanakanda ya Mashariki waweze kufika hapa ili wajifunze mbinu bora za kilimo cha miwa chenye tija” amebainisha Bw. Massamba.
Mojawapo ya vipando vilivyopo katika viwanja J.K. Nyerere kama sehemu ya maandilizi ya Maonesho ya wakulima ya Nanenane yanayotaraji kuanza Agoti 1 mwaka huu.
Naye Bw. Byarugaba Jackson ambaye ni afisa mawasiliano kutoka Mji wa Kibaha ameweka wazi kuwa Maonesho ya Nanenane ya mwaka huu yataenda sambamba na upataji wa elimu, maonesho ya zana za kilimo za kisasa, mbegu bora na kushauri juu ya matumizi sahihi ya teknolojia ya kisasa katika kilimo, ufugaji na uvuvi ili kuweza kuondoa umasikini kwa wakulima hapa nchini.
Bw. Byarugaba Jackson ambaye ni afisa mawasiliano kutoka Mji wa Kibaha akizungumza wakati wa mahojiano.
Kwa upande wake Afisa habari wa Jiji la Tanga Bw. Musa Laban amesema kupitia Maonesho hayo jamii itanufaika moja kwa moja kwani mbinu bora za utunzaji wa mimea hupatikana katika Maonesho hayo hivyo amewananchi hususana wakulima, wafugaji na wavuvi wa Kanda hiyo ya Mashariki kujitokeza kwa wingi kuanzia Agosti mosi kushiriki sherehe hizo katika viwanja vya Mwl. J.K. Nyerere vilivyopo Mkoani Morogoro.
Afisa habari na mawasiliano wa Mkoa wa Tanga akitoa wito kwa wananchi wa kanda hiyo kujitokeza kwa wingi wakati wa sherehe za maonesho ya Nanenane.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.