Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewapongeza wafugaji wa Wilaya ya Mvomero kwa kuwa na mchango mkubwa katika ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Mhe. Malima amesema hayo Juni 13 mwaka huu wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Wilayani MVOMERO.
Mhe. Adam Malima akisalimiana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi - CCM akiwemo Mwenyekiti wa Chama hicho Wilayani Mvomero Ndg. Michael Jaka na Alhaj Sengulo .
Mkuu huyo wa Mkoa amesema, amefurahishwa sana kuona sekta ya mifugo katika Halmashauri hiyo inachangia kwa asilimia kubwa ukusanyaji wa mapato ya ndani kupitia Sekta ya Mifugo
Eneo la mnada wa mifugo uliopo Wilayani Mvomero.
Akisisitiza ukweli huo Mhe. Malima amesema, Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ilifanya makisio ya kukusanya mapato kupitia Sekta ya mifugo na kukusanya shilingi 392,854,000 na kufanikiwa kukusanya jumla ya shilingi 405,624,177 sawa na 103%.
“...sasa nakuambieni wanamvomero, katika Wilaya peke yake ambayo nimeona kidogo ina mchango wa kuridhisha wa wafugaji ni Mvomero...” amesema Mkuu wa Mkoa.
Kwa sababu hiyo amewataka wafugaji katika wa Halmashauri nyingine za Mkoa huo kuiga Mfano huo wa wafugaji wa Mvomero kuwa na mchango wa ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kupitia mifugo yao badala ya kuwa kero kwa jamii na kwa Halmashauri yenyewe.
Katika hatua nyingine Mhe. Adam Malima amewataka Wahe. Madiwani wa Halmashauri hiyo kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao kwa kuwa wao ndio wasimamizi wakuu wa miradi hiyo, hivyo amewataka kuunda kamati itakayofuatilia miradi ya maendeleo.
Baadhi ya Wahe. Madiwani wa Halmashauri ya Mvomero wakiwa kwenye mkutano wa baraza la Madiwani.
Nae Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Bw. Anza Ameni Ndosa kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa huo amewakumbusha Wahe. Madiwani pamoja na watendaji wa Halmashauri hiyo kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kikamilifu na kwa kufanya hivyo miradi hiyo itakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Mipango na Uratibu Bw. Anza Ameni Ndosa (kulia) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mhe. Rebeca Nsemwa ambaye ni kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mvomero.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Yusuph Makunja amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwa na nia njema ya kuibadilisha Halmashauri hiyo na kuwapa nguvu madiwani hao katika usimamizi wa miradi ya maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mvomero Mhe. Yusuph Makunja (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Linno Mwageni wakati wa mkutano wa baraza la Madiwani.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akikagua miundombinu ya barabara Wilayani Mvomero.
Pichani ni baadhi ya majengo ya shule ya sekondari ya Sokoine Memorial.
Muonekano wa jengo la dharura katika hospitali ya Wilaya ya Mvomero.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.