Madiwani wa Halmashauri za Mkoa wa Morogoro wamewatakiwa kuwa na utaratibu wa kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili waweze kujadili hoja hizo kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa hoja za ukaguzi zilizopo katika Halmashauri zao.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam kighoma Malima Juni 26, 2024 wakati akiongoza kikao Maalum cha Baraza la Wahe. Madiwani cha kujadili hoja za CAG kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema, kuna umuhimu kwa wahe. madiwani wa Mkoa huo kujadili hoja za CAG kwa kila vikao wanavyokaa kwa lengo la kuangalia mwenendo wa hoja walizo nazo namna zinavyofanyiwa kazi kwa lengo la kuzifunga, kwani kuwa na hoja nyingi kunaleta doa kwa Halmashauri husika.
"... Kila baraza la madiwani kila linapokaa kwenye vikao vyao lazima kuwe na ajenda ya hoja za CAG.." amesisitiza Adam Malima.
Aidha Mhe. Malima ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kufanya mazungumzo na Jeshi la Magereza Wilayani humo kupata eneo la kutosha lililopo Mikongeni kwa ajili ya kuboresha mnada wa Ng'ombe wa eneo hilo kuwa mnada wenye hadhi ya kimataifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.