Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mhe. Albinis Mgonya amewataka wajasiriamali Mkoani Morogoro kuzalisha bidhaa zenye ubora kisha kihakikisha zinathibitishwa na Wakala wa Viwango Tanzania - TBS ili kuleta ushindani katika soko la ndani nanje ya nchi.
Mhe. Mgonya ametoa kauli hiyo Mei 29, 2021 katika Uzinduzi wa mafunzo ya kusherekea kilele cha kutimiza miaka 10 ya kuanzishwa kwa Taasisi ya GS1 Tanzania ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
‘’TBS Endeleeni kutoa Elimu kwa wakulima na wazalishaji kuhakikisha kwamba wanazingatia viwango vilivyowekwa ili kuzalisha kwa ubora, na tunapotoa Elimu inarahisisha wanapoenda kupata kibali kwenye mamlaka husikawatazingatia vigezo ambavyo vinatakiwa’’ Amesema Mgonya.
Aidha, Mhe. Mgonya amebainisha umuhimu wa Msimbomilia katika bidhaa ni kumsaidia mlaji na wadau wengine kutambua mahali bidhaa ilipozarishwa, kutambua kama bidhaa imethibitishwa na TBS, kusaidia kutambua namna ambavyo bidhaa imetengenezwa na kusaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutambua bidhaa zinazozarishwa kwenye kwenye maeneo yao.
Kwa upande wake Afisa Ufundi wa GS1 Tanzania Ndg. Killian Charles ametoa wito kwa wajasiriamali kuweka Msimbomilia katika biashara zao ili kuzisaidia biashara hizo kufika katika masoko makubwa bila kuwepo usumbufu wowote katika masoko ya ndani na nje.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Asha Rajabu amesema kupitia hutuba ya mgeni rasmi atahakikisha biashara zake anazisajiri TBS na kuhakikisha zinakuwa na Msimbomilia ili kufanya ushindani katika Masoko,
GS1 Tanzania ni Taasisi iliyoanzishwa kwa juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia shirika la utafiti na maendeleo ya viwanda (TIRDO) chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Taasisiya sekta binafsi (TPSF) kwa jukumu la kuziwesha bidhaa za Tanzania kupata utambulisho wake wa alama za mistari Msimbomilia (Barcodes).
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.