WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA ‘WAMKUBALIA RC MALIMA’
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imekubaliana na Maombi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ya kuondoa mifugo ndani ya Pori la Akiba la Kilombero kwa maslahi mapana ya Taifa.
Wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge walifika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo Wakiwa katika ziara yao ya kikazi na Mhe. Mkuu wa Mkoa hupo kutoa mapendekezo yake na wao kumhakikishia Mkuu huyo kulitafutia ufumbuzi tatizo la uingizaji wa mifugo katika pori hilo.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vita Rashidi Mfaume Kawawa ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Uchaguzi la Namtumbo, amesema wanajua changamoto hiyo ya mifugo katika bonde hilo na kwamba baadhi ya mifugo hiyo ni kutoka nchi Jirani, hivyo wataenda kulisemea suala hilo Bungeni.
Mambo mengine ambayo Mkuu wa MKoa wa Morogoro aliwaomba Wahe. Wabunge wa Kamati hiyo kuyasemea bungeni ni pamoja na suala la kuthibiti mafuriko ndani ya Mkoa wa Morogoro na kupunguza kasi ya Mmomonyoko wa maadaili ndani ya jamii.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.