Wakaguzi wa ndani Mkoa wa Morogoro wametakiwa kushirikiana na wa Halmashauri pamoja na Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri zao ili kuhakikisha zoezi la Anwani za Makazi na Posti Kodi linaloendelea nchi nzima linafanikiwa kama maagizo ya Serikali yalivyoelekezwa.
Ushauri huo umetolewa Aprili 28 mwaka huu na Mkaguzi wa Ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Benedict wakati akifungua mafunzo ya wakaguzi wa Ndani yaliyofanyika katika ukumbi mdogo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mafunzo hayo ambayo pamoja na kutaka kuwajengea uwezo Maafisa hao kwa ajili ya kutekeleza vema majukumu yao ya kila siku kwenye Halmashauri zao pia yalilenga kushiriki kwa asilimia mia katika kushauri na kukagua matumizi ya fedha za Serikali zilizizoelekezwa kwenye zoezi la Anwani za Makazi na Posti Kodi.
Baadhi ya wakaguzi wa ndani wakiwa kwenye kikao hicho cha siku moja
Hata hivyo amewataka wakaguzi hao watoe ushirikiano kwa viongozi wao katika kutekeleza zoezi hilo kwa ufanisi na sio kusababisha changamoto itakayosababisha kukwamisha zoezi hilo.
“Kwa hiyo twende tukawasaidie waone kwamba sisi ni msaada kwao na sio changamoto…kwa hiyo twende kwenye mlengo huo wa kufikia malengo” amesema.
Mkaguzi wa Ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Benedict (kushoto) akisikiliza kwa makini mafunzo yanayotolewa na Afisa TEHAMA Mhandisi Rhobison Deus (kulia).
Akiongea baada ya mafunzo hayo Mratibu Msaidizi wa Zoezi la Anwani za Makazi na Posti Kodi Mkoa wa Morogoro Kayombe Masoud Rioba amesema Mkaguzi wa ndani ni jicho la pili la kila taasisi hivyo kuna umuhim wa Maafisa hao kuwepo kwenye zoezi la Anwani za Makazi kwa kila Halmashauri ili kushauri na kusimamia matumizi ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya zoezi hilo.
Kwa upande wa zoezi lenyewe la Anwani za Makazi Rioba amesema zoezi hilo linaendelea vizuri na kwa sasa Mkoa huo umejikita kwenye usajiri wa miundombinu na zoezi hilo linategemea kukamilika tarehe iliyopangwa yaani Mei 15 mwaka huu.
wakaguzi wa ndani wakiwa katika picha ya pamoja mara baaada ya kukamilika kikao hicho
Nao wanamafunzo hayo akiwemo Bakari Luguguda Kaimu Mkaguzi wa Ndani Wilaya ya Ulanga amesema kama wadau wanaishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuratibu kikao kazi hicho akibainisha kwamba Kikao hicho kitawasaidia Wakaguzi wa ndani kugagua fedha zinazotumika kwenye zoezi Anwani za Makazi lengo ni sote ka pamoja kukamilisha kwa ufanisi zoezi hilo.
Mkaguzi wa Ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa amewataka wakaguzi wa ndani wa Halmashauri zote kufanya kazi kwa uaminifu kama ambavyo Serikali ina wategemea na kuwaona kama jicho la matumizi hayo ya fedha basi wao pia wafanye kazi hiyo inayotazamiwa na Serikali kuanzia kwenye utekelezaji wake hadi kwenye masuala ya matumizi yake.
Mkaguzi wa Ndani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Stephen Benedict akiongea na wakaguzi wa ndani waliohudhuria kikao hicho
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.