• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Wakulima Malinyi watakiwa kuuza mazao kwa mfumo wa stakabadhi gharani.

Posted on: June 6th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh. Adam Malima akiangalia hali ya zao la mahindi Wilayani Malinyi.

Wananchi wa Wilaya ya Malinyi wametakiwa kuuza mazao yao hususan zao la ufuta kwa kutumia mfumo wa stakabadhi Gharani kwa lengo la kumsaidia mwananchi kutonyonywa na wafanyabiashara wasiowaaminifu wanaonunua zao hilo kwa bei ya chini hivyo kumletea mkulima umaskini.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa MKoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima Juni 5 mwaka huu wakati wa ziara yake ya kikazi ya  kutembelea miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi kwa Halmashauri zote tisa za Mkoa huo.

Hapa Mhe. Adam Malima (wa kwanza kushoto) akimsikiliza mtaalamu wa kilimo.

Siku ya kwanza ya ziara hiyo akiwa Wilayani Malinyi Mhe. Adam Malima amekutana na kile wananchi wanachokiita kero ya kuuza zao la ufuta kwa mfumo wa stakabadhi gharani huku baadhi yao wakionesha ama kutouelewa vema umuhim wake au wachache wamerubuniwa na wafanyabiashara kutoupokea utaratibu huo kwa maslahi yao binafsi.

kwa sababu hiyo, Mkuu huyo amewataka wakulima wa Wilaya hiyo kufuata mfumo wa stakabadhi gharani wanapouza zao hilo lengo ni kumnyanyua mkulima mdogo na sio kumnyonya kwani amesema kwa mfano bei ya zao hilo kwa siku ya Juni 7, 2023 kupitia mfumo huo ni shilingi 3,400 kwa kilo moja badala ya shilingi 2,800 kwa kilo moja kwa kuuza nje ya utaratibu huo.

"sasa mimi wajibu wangu kama Mkuu wa Mkoa ni kuhakikisha kuwa mkulima yule ambaye anaingizwa usiku nimlinde... mimi ninachotaka kwamba mtu atakapoenda kununua ufuta aangalie bei ambayo mkulima angepata kwenye stakabadhi gharani ampe hiyo" amesisitiza Mhe. Adam Malima.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima alipata nafasi ya kukagua miundombinu ya barabara Wilayani humo.

Katika hatua nyingine, akiwa bado Wilayani humo Mkuu wa Mkoa amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Malinyi kumtaka Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo kutoa Elimu ya Kilimo chenye tija kwa wananchi wake badala ya kuwaacha kuendelea na kilimo cha mazoea na kisicho na tija katika uzalishaji huku akishangaa namna ardhi nzuri na yenye rutuba iliyopo Wilayani humo kutotumika ipasavyo.

Aidha, Mhe. Adam Malima amewataka wananchi wa Malinyi kuacha migogoro isiyo na faida na kumsababisha yeye kuhangaika na mambo madogo badala ya kushughulikia mambo makubwa kama masuala ya barabara ambayo kwake amesema ni kipaumbele cha kujenga hoja ili kuondoa kero hiyo inayosababisha wananchi kukwama njiani na kuwacheleweshea maendeleo yao.

MWISHO.




Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.