RC Morogoro achangia mifuko 50 ya Saruji kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kibwaya
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela ameunga mkono juhudi za wananchi wa Kijiji cha Kibwaya kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mkoani humo kwa kuchangia mifuko 50 ya saruji baada ya wananchi hao kujenga boma la zahanati kwa nguvu zao.
RC Martine Shigela
Martine Shigela amefikia hatua hiyo Juni 22 mwaka huu alipoutembelea mradi huo na kuridhika na ubora wa jingo hilo pamoja juhudi za wananchi za kujenga zahanati hiyo ambayo iko katika hatua ya umaliziaji huku wakianza ujenzi wa nyumba ya mganga jambo lililomsukuma Kiongozi huyo kuchangia mifuko 50 ya saruji.
“Sasa madamu mmejitolea na mimi nitawachangia mifuko ya simenti hamsini ili ujenzi huo uanze mara moja, kwa hiyo shukrani hizo tutamfikishia Mhe.Rais na ninyi mnajua siku zote mwenye nacho ndiye anayeongezewa” amesema Martine Shigela.
jengo la zahanati lya Kibwaya ililojengwa kwa nguvu za wananchi wa kijiji hicho likiwa kwenye hatua za umaliziaji
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kibwaya akiwemo Bw. Juma Kisiga wamemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapelekea fedha shilingi milioni 50 za kumalizia jengo la zahanati ambalo walianza kujenga mwaka 2010 na kukamilika mwaka 2013 bila mwendelezo wowote hadi sasa Mhe. Samia alipopeleka fedha za kumalizia jengo hilo.
“Hili jengo lilianza kujengwa mwaka 2010 likaisha 2013, tangu hapo likakaa kimya mpaka sasa awamu hii ya Mama Samia ndio kazi hii inaendelea kufanyika tena kwa ubora, juu ya hilo tunaomba salamu za asante zifike ngazi zote za Serikali zilizoshiriki kutufanikishia jambo hili” amesema Bw. Juma Kisiga.
Mhe. Shigela akikagua ujenzi wa Jengo la Zahanati ya Kibwaya
Katika hatua nyingine, wananchi wa Kijiji hicho wamelalamikia mradi wa maji uliojengwa kijijini hapo na kugharimu Shilingi 610,000,000/= ulioanza kujengwa tangu mwaka 2015 lakini mradi huo bado hauna tija kwa wakazi wa eneo hilo kwa kuwa maji yanatoka kwa kusua sua.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mhe. Lucas Lemomo akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Rehema Bwasi
Sehemu ya Wahe, Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro wakiwa kwenye kikao Maalum cha kujadili hoja za Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG Juni, 22 2022
Kwa sababu hiyo, Mkuu wa Mkoa Martine Shigela amewatahadharisha wote wanaotuhumiwa kuhusika na ujenzi wa mradi huo wa maji na kwamba kama maelezo yaliyotolewa na wananchi yako sahihi, basi wajiandae kuzitapika fedha zote za mradi huo walizozitafuna.
kutoka Kushoto, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Albert Msando, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Martine Shigela na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Mhe. Lucas Lemomo, wakiwa kwenye kikao muda mfupi kabla ya kutembelea jengo la zahanati ya Kibwaya
Ameongeza kuwa, Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan ina dhamira ya dhati ya kumtua mama ndoo kichwani na kwa kuwa makosa ya jinai hayaozi wahusika wa mradi huo watatafutwa ili wakamilishe mradi huo ili ulete tija kwa wananchi.
Hata hivyo, amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa huo kufuatilia kwa karibu changamoto za mradi huo kupitia kwa kwa Wakala wa Maji Mijini na Vijijini RUWASA ili kujua tatizo haswaa la mradi huo kutotoa maji.
Kushoto, ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bi. Mariam Mtunguja
Baadhi ya watendaji wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro, katikati ni Dr. Rozaria Rwegasira Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalrishaji Mali kulia ni Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Serikali za Mita Bw. Leopord Ngirwa
Baadhi ya Viongozi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Morogoro (DAS), Afisa Usalama wa Taifa Wilaya (DSO) na Kamanda wa Polisi wa Wilaya hiyo (OCD)
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.