• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WANATUHUMIWA KUUZA MALI ZA USHIRIKA MOROGORO.

Posted on: June 7th, 2025



Wajumbe watano wa Bodi ya chama cha Ushirika Mkoa wa Morogoro (MOFACU) kwa kushirikiana na Meneja wa Chama Kikuu cha Ushirika huo wamefikishwa kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kuuza mali za ushirika huo bila kufuata taratibu wa Ushirika huo.

Watuhumiwa hao wamechukuliwa hatua hiyo kufuatia uchunguzi ulioanzishwa kuhusu uuzaji wa ghala la chama hicho kwa bei ya chini ukilinganisha na thamani halisi, pamoja na uuzaji wa vyuma chakavu bila kuthaminisha mali hizo.

Akizungumza Juni 7, 2025, katika kikao cha uchaguzi wa wajumbe wapya wa MOFACU kilichofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Morogoro, Bi. Cesilia Sostenes, alieleza kuwa uuzaji huo ulikiuka muongozo wa mwaka 2024 unaoelekeza mali za ushirika kuuzwa baada ya kupitishwa na mkutano mkuu, kuthaminiwa, na kupata kibali kutoka kwa Mrajisi.

"Mali hii imeuzwa na wajumbe wa Bodi bila kufuata taratibu. Tunaendelea kufuatilia kwa sababu kesi ipo TAKUKURU kwa ajili ya uchunguzi kama kulikuwa na mazingira ya rushwa ili hatua ziweze kuchukuliwa," alisema Bi. Sostenes.

Kwa mujibu wa mthaminishaji wa mali, ghala hilo lilikuwa na thamani ya shilingi milioni 126 lakini liliuzwa kwa shilingi milioni 56 tu. Aidha, vyuma chakavu viliuzwa kwa shilingi milioni 6 bila kufanyiwa uthamini.

Mwakilishi kutoka Chama cha Ushirika cha Msingi Dakawa Bwakila Amkosi, Bw. Salum Mohamed, alieleza kuwa ghala hilo lilipendekezwa kuuzwa kwa kufuata sheria zote ili fedha itakayopatikana ilipe chama cha ushirika cha zamani. Hata hivyo, kama limeuzwa bila utaratibu, ni kosa.

Naye mwanachama wa MOFACU, Bw. Mohamed Salum, aliwakumbusha wanaushirika umuhimu wa viongozi kushirikisha wanachama wote wa chama ili kupata maoni na kujua kuwa mali inauzwa na kujua bei inayotakiwa kuuzwa ili kuepusha ubadhirifu wa mali za wanaushirika.

Watahumiwa wanaendelea kuhojiwa na TAKUKURU ili kujiridhisha ukweli wa jambo hilo.


MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WANATUHUMIWA KUUZA MALI ZA USHIRIKA MOROGORO.

    June 07, 2025
  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.