Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2021 Lt. Josephine Mwambashi amewataka wasimamizi wa miradi inayopitiwa na mwenge kote nchini kuwasilisha nyaraka za miradi wakati wa ukaguzi ili kuepusha usumbufu unaojitokeza mara kwa mara.
Kiongozi huyo ametoa agizo hilo Agosti 6, 2021 Wilayani Malinyi kabla ya kuzindua na kuweka jiwe la msingi katika Ofisi ya Udhibiti ubora iliyojengwa kwa fedha za Serikali.
Lt. Mwambashi amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya wasimamizi wa miradi ya inayopitiwa na mwenge huo kushindwa kuwasilisha nyaraka muhimu wakati wa ukaguzi wa miradi licha ya kutoa taarifa kwa wasimamizi hao kabla ya kufika eneo la tukio.
‘’Tuwe makini na miradi tuwe makini na nyaraka, tafuta faili na uambatanishe nyaraka zote zinazohitajika ili tukija kuangalia tunafunua ndani na kukuta taarifa zote. Tunapoteza muda mwingi katika baadhi ya miradi kwa sababu ya kukosekana kwa nyaraka’’ amesema Lt. Mwambashi.
Aidha, Lt. Mwambashi ametoa onyo kali kwa wasimizi wa miradi ya maendeleo kuhakikisha katika nyaraka zao wanabainisha matumizi sahihi ya ujenzi wa miradi hiyo ili wakati wa ukaguzi usiwepo ubabaishaji ambao unapelekea kutofunguliwa ama kuzinduliwa kwa miradi inayokusudiwa.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.