Watoa huduma za kisheria kwenye kampeni itakayozinduliwa kesho ya Mama Samia Legal AID wametakiwa kuzingatia miongozo ya utumiaji huduma, kutoa huduma kwa wananchi kwa kuzingatia ufanisi, weledi, usawa na bila upendeleo.
Wito huo umetolewa leo Disemba 12, 2024 na Katibu Tawala Msaidizi Section ya Miundombinu Mkoa wa Morogoro Mhandisi Ezron Kilamhama wakati akifungua mafunzo ya kuwajengea uwezo wataalamu hao kutoka kada mbalimbali katika kughulikia changamoto za kisheria kwa wananchi.
Akiongea katika mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro idha Mhandisi Kilamhama amesema ni jukumu la kila mtaalam kwenda kushughulikia changamoto za wananchi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kusuluhisha migogoro mbalimbali na kutoa elimu juu ya sheria mbalimbali ili waweza kuondoa changamoto zinazowakabili.
".. Wananchi wengi wanahitaji sana hii huduma ambayo mnaenda kuifanya, isijitokeze miongoni mwetu tukaanza kutumia njia kinyume na sheria katika kutoa huduma hiyo."
Sambamba na hayo kiongozi huyo amesema, mafunzo hayo yanajumuisha wataalamu mbalimbali wakiwemo maafisa ardhi, wanasheria, maafisa maendeleo ya jamiii, na dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi, mawakili wa kujitegemea, na wasaidizi wa sheria, hivyo kupitia viongozi hao elimu na huduma zitatolewa kwa ufanisi mkubwa.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uelewa wa pamoja kuhusu msaada wa Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia "Mama Samia legal AID Campaign" pia kufahamu majukumu ya kila mmoja kuandaa utoaji huduma wa msaada wa kisheria ambapo kupitia mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao ya kikazi ipasavyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Msaada wa Kisheria Bi. Ester Msambazi amesema mafunzo hayo watakayoyapata wataalamu hao yataenda kuwasaidia kutoa huduma ndani ya siku 9 kuanzia Disemba 14 hadi 22, 2024 katika Mkoa wa Morogoro ikiwezo kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.
Naye mwanasheria kutoka Halmadhauri ya Wilaya ya Ulanga Bw. Elikarim Samwel amesema mafunzo hayo aliyoyapata yataenda kumasaidia katika kutatua changamoto hususan migogoro ya wakulima na wafugaji na kusuluhisha migogoro ya mirathi katika familia.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.