• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Watumishi wa Mahakama Watakiwa Kufanya Maandalizi ya Kustaafu.

Posted on: July 27th, 2021

Wtumishi wa mahakama kote nchini wametakiwa kufanya maandalizi  ya mapema kabla ya kustaafu ili kutengeneza mazingira mazuri yatakayowasaidia baada ya kupewa fedha zao.

Kauli hiyo imetolewa Julai 26 mwaka huu na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu  wa Mahakama ya Tanzania Bw. Edward Nkembo wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa mahakama ya Tanzaniya  yanayofanyika kwa siku tano katika ukumbi wa Magadu uliopo katika halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Nkenda amesema ni vyema mtumishi kuweka mipango mkakati ya kufanya maandaliza ya kustaafu tangu anapoajiriwa ikiwa ni pamoja na kuainisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo ambayo haitawapelekea kuwa tegemezi.

Aidha, Nkenda amebainisha kuwa wastaafu wengi wamekuwa wakiishi muda mfupi baada ya kustaafu kutokana na matumizi mabaya ya fedha zao ambapo mara nyingi fedha hizo huzitumia kinyume na utaratibu ambao wanakuwa wamejiwekea kabla ya kustaafu.

‘’Changamoto kubwa zinazowakabili watumishi baada ya kustaafu ni kushindwa kupata mahitaji ya lazima, kutapeliwa mafao yao, kupokea maoni mbalimbali ya kufanya biashara ambazo zinamaliza pesa zao na kubadili tabia zao kisha kuishi maisha ya starehe’’ amesema Nkenda.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mafunzo hayo kutoka Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Ndg. Nuhu Mtekele amesema pamoja na mafunzo watakayopatiwa katika semina hiyo, washiriki hao watapata fursa ya kutembelea Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo – SUA kilichopo Mkoani humo ili kujionea kwa vitendo miradi na shughuli za ujasiliamali na uwekezaji katika kilimo, uvuvi  na ufugaji.

Ndg. Mtekele amesema kufanya ziara katika Chuo hicho kutawajengea uwezo watumishi hao  kutambua aina ya kazi ambayo wanaweza kuifanya mara baada ya kustaafu ili kuwaletea maendeleo binafsi pamoja na jamii iliyowazunguka  kwa jumba.

Kwa upande wake Nestory Mujunangoma, ambaye ni Mtendaji wa Mahakama Mkoa wa Morogoro ametoa rai kwa  watumishi hao kutojihusisha katika miradi mikubwa ambayo watashindwa kuiendesha na badala yake wajikite katika  miradi  midogo  ikiwa ni pamoja na ujasiliamali ambao utawaletea faida kubwa ya kujikwamua na umaskini.

Sambamba na hayo, amewashauri watumishi hao kujali Afya zao, kuepuka madeni yasiyo ya lazima, kutoendekeza anasa na kuishi vizuri katika jamii ili thamani ya kustaafu iweze kuonekana mbele ya familia zao na Jamii kwa jumla.

Mafunzo hayo ya siku tano ya kustaafu ni sehemu ya utekelezaji wa sera wa mafunzo ya utumishi wa umma ya mwaka 2013, Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania, Sera ya Mafunzo ya Mahakama ya Tanzania ya Mwaka 2019 pamoja Mpango Mkakati wa Chuo wa Miaka mitano wa Mwaka 2018/2019 hadi 2020/2023.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.