• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Wauguzi nchini watakiwa kutoa huduma nzuri na majitoleo.

Posted on: January 7th, 2024

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amewataka Wauguzi wote hapa nchini kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa, ukarimu na kuwa na majitoleo ili kundoa lawama za wananchi zinazoelekezwa kwa Serikali.

Mhe. Mchengerwa ametoa agizo hilo Januari 8 mwaka huu wakati akikabidhi magari 6 kwa Mganga wa Mkoa wa Moroboro na Halmashauri za Mkoa huo makabidhiano  yaliyofanyika hoteli ya Glonency iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Mhe. Mchengerwa amesema, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kuboresha maslahi ya wauguzi hapa nchini hivyo amewataka kuwahudumia wagonjwa kwa ukarimu, bidii na kutanguliza  majitoleo katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa hususan wajawazito kama alama ya shukrani kwa Rais Samia.

"...niwaombe sana mkaishi katika maono ya Dkt. Samia Suluhu Hassan...tunategemea ninyi mkafanye kazi nzuri katika maeneo yenu...wahudumieni watanzania, wakija wakina mama wajawazito wahudumieni kwanza maswali baadaye .." amesema Waziri Mchengerwa.


Aidha, amewataka Waganga wa Mkoa na wa Halmashauri hapa nchini kuyatumia magari waliyopewa kwa malengo yaliyokusudiwa na Serikali ya kufuatilia na kusimamia huduma za Afya katika maeneo yao pamoja na kusikiliza kero za wauguzi wao na kuzitatua.

Akibainisha ununuzi wa magari hayo Mhe. Mchengerwa amesema magari hayo yamegharimu shilingi bilioni 52.38 kwa ajili ya Waganga wakuu wa Mikoa na waganga wakuu wa Wilaya huku akibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hadi sasa imenunua kwa mpigo magari 528 ya kuhudumia wagonjwa huku kukiwa na mpango wa kununua magari ya kubebea wagonjwa "ambulance" kwa kila jimbo la uchaguzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima  amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutowaacha nyuma  wananchi wa Mkoa huo hususan katika Sekta za Maji, Afya na Elimu na kumuomba Waziri Mchengerwa kufikisha shukrani za wanamorogoro kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akiahidi kuwa Mkoa unaenda kuongeza kasi ya ufanisi kupitia rasilimali anazozitoa kwa wananchi wa Mkoa huo.

Magari yanayotolewa sasa ambapo kwa Mkoa wa Morogoro umepata magari 6 ni mgao wa awamu ya kwanza ambapo Waganga wa Halmashauri za Morogoro, Kilosa, Malinyi na Ulanga zimepata magari hayo pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.