WAVAMIZI VYANZO VYA MAJI KUONDOLEWA
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa ameagiza mamlaka zinazohusika na utunzaji wa vyanzo vya maji kuwaondoa Mara moja wavamizi wote katika maeneo ya vyanzo vya maji ili kuhakikisha kuwa vyanzo hivyo vya maji vinabaki salama kwa manufaa ya watanzania wote.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa (katikati) akiwa kwenye kongamano la wadau wa kilimo, kushoto ni Dr. Rozalia Rwegasira Katibu Tawala msaidizi-Uchumi, kulia ni Mwenyekiti wa kongamano hilo Profesa Paramagamba Kabudi(M).
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo septemba 28 mwaka huu wakati akifungua Kongamano la Wadau wa Kilimo Mkoa wa Morogoro, kongamano ambalo lililenga kujadili maendeleo ya kilimo, Mifugo na Hifadhi za Mazingira, kilichofanyika Katika Hoteli ya Morena iliyopo Manispaa ya Morogoro.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi katika Mkoa huo kushirikiana Ili kutatua changamoto za wananchi wanao waongoza na kuwasimamia Ili kuleta maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Hanji Godigodi pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngolo Malenya wakiwa kwenye Konamano hilo.
Amesema, kukosekana kwa mshikamano na ushirikiano wa viongozi kuna sababisha utendaji wao kukosa ufanisi na wananchi kutokuwa na imani na viongozi wao.
Wajumbe wa Kongamano hilo wameazimia kutoa elimu kwa wakulima Ili waweze kufuata ushauri wa wataalam wa Kilimo na kuondokana na kilimo kisicho na tija na kinachosababisha athari za mazingira kama vile uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji, ukataji wa miti ovyo hali inayosababisha ukame na athari nyingine hivyo kuathiri sekta ya utalii na Maliasili zilizopo katika mkoa huo.
Kongamano Hilo lihirikisha Viongozi mbalimbali wakiwemo, Katibu tawala wa Mkoa wa Morogoro, Wakuu wa Wilaya, Wabunge, Wenyeviti wa Halmashauri Wataalamu wa Kilimo, maji na mazingira, wakulima na wafugaji.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na Wilaya wakiwa kwenye Kongamano.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.