Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ameagiza Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Morogoro (MORUWASA) na Bodi ya maji, Bonde la Wami Ruvu kuhakikisha wanashirikiana kuondoa majani yaljyoota juu ya maji katika bwawa la mindu ambalo linategemewa na wakazi wa manispaa ya morogoro kwa ajili ya maji na shughuli nyingine za kijamii.
Waziri Aweso ametoa agizo hilo Julai 23, 2024 wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja ambapo alitembelea bwawa hilo lililopo kayika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani humo ambapo pia katika ziara hiyo ametembelea Wilaya ya Gairo.
".. Hili bwawa ndio roho ya wanamorogoro, ukisikia roho ya wanamorogoro ni hili bwawa la mindu.."
Mhe. Aweso Amesema, kutokana na majani hayo yaliyota juu ya maji, inaonesha kutokuwa na usimamizi mzuri wa utunzaji wa mazingira ya bwawa hilo hivyo amezitaka mamlaka husika kuhakikisha bwawa hilo linafanyiwa usafi mara kwa mara ili kuepuka majani kuendelea kuota juu ya maji.
Pia Waziri huyo mwenye dhamana ya maji amesema katika bwawa hilo kuna uwepo wa makazi ya watu hivyo ametaka kushirikiana na viongozi eneo hilo kwa kuwaondoa wakazi wote waliojenga karibu na bwawa hilo huku akibainisha kuwa wakazi ambao nyumba zao zimefanyiwa tathmini watalipwa fidia.
Aidha Mhe. Aweso ametoa agizo kwa viongozi wa Wizara hiyo ndani ya wiki moja kutafuta gari na kuwapatia wataalam wanaosimamiz Ubora wa mai kutoka Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Morogoro ( MORUWASA) ili kuwezesha wataalam hao kufika katika miradi ya maendeleo hususan ya Maji kwa urahisi na kuweza kutoa huduma ya Maji safi kwa wananchi.
Katika hatua nyingine, Mhe. Aweso ametoa wito kwa viongozi wa MORUWASA kutokaaa maofisini wakati wa kazi badala yake waende kwenye miradi ya maendeleo kukagua miradi hiyo ili kuweka msukumo wa kukamilika kwa mirad8 hiyo kwa wakati na ubora unaotakiwa.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.