WAZIRI BASHUNGWA ATOA MIEZI MIWILI KWA WAKANDARASI
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa amemuagiza mkandarasi anayejenga Barabara ya Kidatu – Ifakara kwa kiwango cha lami, yenye urefu wa Km 66.9 inayojumuisha ujenzi wa Daraja la mto Ruaha, lenye urefu wa Mita 133 kukamilisha ujenzi huo ndani ya mienzi miwili kuanzia Februari 23 mwaka huu.
Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo Februari 23, 2024 wakati wa ziara yake ya siku Nne Mkoani Morogoro ambapo Februari 23, 2024 amefanya ziara katika Wilaya ya Kilosa na Kilombero na kutembelea miradi mbalimbali ya Barabara na madaraja.
Akikagua ujenzi wa Daraja la mto Ruaha, Waziri Bashungwa amesema hataki kusikia wala kupelekewa ombi la kuongezewa tena muda kwa kwa kisingizio cha mvua kwa kuwa amesema Mkandarasi wakati anaweka mkataba huo walijua pia kuwa kuna kipindi cha kiangazi na kipindi cha mvua.
“ kama nilivyosema sitaki Additional cost kwa sababu ya mvua, kwa sababu mkandarasi wakati anaweka mkataba alijua kuwa mvua zitanyesha” amesema Mhe. Bashungwa.
Waziri amebainisha kuwa Daraja hilo litafungua uchumi wa wakazi wa Mikoa ya Morogoro, Njombe, Iringa na Ruvuma kwa kuwa Barabara hiyo inapita kwenye eneo lenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara.
Hata hivyo amesema maono ya Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kutaka Barabara hiyo ianzie Bandari ya Tanga hadi Mkoa wa Njombe kupitia Turiani, Dumila Rudewa na Kilosa Mjini. Aidha, Barabara hiyo ambayo inajengwa kwa awamu itaendelea Kwenda Mikumi, Ifakara, Mbingu hadi Kibena na Lupembe Mkoani Njombe.
Akiwa Wilayani Kilombero Waziri Bashungwa ametembelea mradi wa Barabara ya Ifakara - Mbingu yenye urefu wa km 62.5 ambapo pia ametoa miezi miwili kwa Kampuni ya HENAN kutoka nchini China, kuhakikisha analeta mitambo, watumishi na vifaa vingine muhim ili kuanza ujenzi wa Barabara hiyo mara moja.
Kwa upande wake Mkuu wa MKoa wa Morogoro Mhe. Adam Kigoma Malima amesema, ujenzi wa Daraja la mto Ruaha ni muhim sana kwa Uchumi wa nchi na ndio maana Mkoa pia unaufuatilia kwa karibu na kuusimammia kwa nguvu zote.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.