WAZIRI MHAGAMA ATEMBELEA WAATHIRIKA WA MVUA MOROGORO,
APONGEZA NA KUTOA MAAGIZO
Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu - Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama ametaka elimu iendelee kutolewa kwa wananchi kuhusu madhara yanayoweza kutokea kutokana na mvua nyimgi zinazoendelea kunyesha hapa nchini na kwamba mvua hizo zitaedelea kunyesha hata baada ya kipindi hiki cha vuri.
Waziri Mhagama ameto kauli hiyo Januari 26, 2024 akiwa Mkoani Morogoro na kutembelea maeneo mbalimbali yaliyoathiriwa na Mvua zilizonyesha Januari 25, 2024 na kusababisha vifo vya watu, uharibifu wa miundombinu Pamoja na upotevu wa mali za wananchi.
Katika hatua nyingine, Pamoja na kutaka watendaji wa serikali Mkoani Morogoro wakiwemo TARURA, TANROAD, TANESCO, RUWASA na MORUWASA kujipanga kurudisha miundombinu iliyoharibika na kuwa tayari wakati wote katika kipindi hiki cha mvua, amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Pamoja na timu yake kwa kujipanga vizuri kukabiliana na changamoto za mvua zinazoendelea kunyesha.
Amesema, Mkoa kwa kuanzisha kikundi cha kusaidia wahanga - Fire Volunteers ni dalili kuwa Mkoa umejipanga na akatumia fursa hiyo kukipongeza kikundi cha Fire voluntires kwa kazi nzuri waliyoifanya Januari 25, 2024 ya kuokoa watu na mali zao huku Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akamuomba Waziri Mhagama kuliongezea nguvu jeshi la Zima Moto na Uokoaji ili kuimarisha vijana hao wa fire Fire Volunteers.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.