Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) amemtaka Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri wa Fedha na Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA kukaa kwa pamoja na kutatua matatizo yaliyopo baina yao ili kuruhusu makonteina yaliyopo bandarini kwa ajili ya ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mbigiri.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo Agosti 14 mwaka huu wakat wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya kiwanda cha Sukari cha Mbigiri kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
“….Kaeni kwa haraka na mfanye maamuzi ya kutoa makontena ili taratibu zingine ziendelee, ujenzi hapa usikwame na kwa kufanya hivyo bodi haitopata hasara wala mkandarasi hatochelewa kukamilisha hatua alizojipangia’’…amesema Majaliwa.
Bonyeza link hii hapa chini kuangalia video hii katika YouTube channel yetu.
https://www.youtube.com/watch?v=Q910u_9s_C0
Tafadhali share, comment na subscribe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.