• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Waziri Mstaafu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda aitaka Nanenane Kanda ya Mashariki kutumia vema fursa.

Posted on: August 5th, 2022

PINDA AITAKA NANENANE KANDA YA MASHARIKI KUTUMIA VEMA FURSA

Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Taznania Mizengo Kayanza Peter Pinda amesema fursa nyingi za kiuchumi zilizopo katika Kanda ya Mashariki ya maonesho ya Nanenane zitasaidia kupiga hatua kubwa kiuchumi endapo zitatumika ipasavyo.

Mizengo Pinda ameyasema hayo Agosti 4,  2022 alipokuwa anafungua rasmi maonesho ya wakulima maarufu kama nanenane kanda ya Mashariki inayoundwa na Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na wenyeji Morogoro.

Akitoa hotuba yake ya ufunguzi mara baada ya kutembelea mabanda ya bidhaa mbalimbali katika Maonesho kwenye viwanja vya vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Nanenane Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Waziri Mkuu amesema Kanda ya Mashariki ina fursa lukuki za kiuchumi na hivyi inaweza kupiga hatua ya haraka kiuchumi.


“sidhani kama kuna Kanda nyingine ambayo iko katika hali nzuri ya kuweza kukua kwa haraka kuliko Kanda ya mashariki, kanda hii ndio inakodolea Mlango wa bandari ya Dar es Salaam” amesema Waziri Mkuu Mstaafu.


Akifafanua zaidi amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na Bandari za Dar es Salaam na Tanga, uwepo wa ujenzi wa Bomba la mafuta la kutoka Tanga kwenda Uganda, uwepo wa Reli ya mwendo kasi na miundombinu ya barabara za Lami.

Fursa vyingine alizozitaja ni pamoja na uwepo wa vyuo Vikuu vinavyopatikana katika kanda hiyo, kasi ya ukuaji kiviwanda katika Mkoa wa Pwani pamoja na idadi ya wakazi wake wa mikoa hii minne ambao wako zaidi ya milioni 13 sawa na zaidi ya asilimia 21 ya watanzania wote ambao tayari ni soko tosha kwa kanda hii.


Katika hatua nyingine amewataka Viongozi wa Kanda hiyo kuyafanya maonesho ya kanda hiyo kuwa na matokeo kwa wananchi kutokana na maarifa yanayopatikana katika kipindi chote cha maonesho ya nanenane, badala ya kuishia viwanja vya nanenane Morogoro maarifa hayo yashuke kwa wananchi.


Hata hivyo amegusia matumizi ya vyuo vikuu vilivyopo katika Kanda hiyo kikiwemo Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoinne – SUA kupata tafiti zake kuhusu kilimo na kuzitumia badala ya tafiti hizo kubaki kwenye makaratasi.

Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki yeye alisisitiza suala nzima la kuongeza juhudi ya kuwapa watanzania elimu kuhusu kilimo, kufuga na kuvua kwa kutumia njia bora na za kisasa zaidi.

Aidha, Mashimba Ndaki ametumia jukwaa hilo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kibali cha kuajiri maafisa ugani wa mifugo 300 na kuruhusu bajeti ya kununua pikipiki 1,300 kwa ajili ya Maafisa ugani ngazi ya Kata.

Awali akiwakaribisha wageni hao, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa, nje ya kuahidi kutekeleza maagizo aliyoyatoa Mgeni rasmi wakati wa kutembelea mabanda, Mkuu huyo wa Mkoa wa Morogoro amewahakikishia wanamorogoro na watanzania wote kwa jumla kuutumikia Mkoa huo kwa juhudi zake zote na kwamba matamanio yake ni kuupaisha Mkoa huo.

MWISHO 


 

 

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.