• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAZIRI WA KILIMO ZANZIBAR AAHIDI KUSHIRIKIANA NA MKOA WA MOROGORO.

Posted on: August 4th, 2023

Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Shamata Shaame Khamis amesema Wizara yake ipo tayari kushirikana na wataalam, wakulima na viongozi wa Mkoa wa Morogoro katika kuongeza uzalishaji wenye tija wa mazao ya kimkakati hususan zao la karafuu kwa lengo la kuinua uchumi wa wakulima na taifa kwa ujumla.


Mhe. Shamata ameyasema hayo Agosti 3, 2023 alipotembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya Morogoro ambayo inalima zao karafuu wakati alipotembelea mabanda ya maonesho ya Nanenane yanayofanyika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjini Morogoro.

Hili ni zao mchikichi ambalo ni miongoni mwa mazao yanayolimwa katika Halmashauri ya Morogoro.

Aidha, Mhe. Shamata Khamis amesema kutokana na umuhimu wa zao hilo katika kukuza kipato cha wakulima na taifa, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya kilimo itashirikiana na Mkoa wa Morogoro kwa karibu zaidi na kuhakikisha mazao hayo yanakuwa na tija.

Huyu ni mkulima wa zao la vanila akielezea mchakato wa uzalishaji wa zao hilo.

Kwa msingi huo, Wizara hiyo inatoa nafasi kwa wataalam na wakulima kutoka Mkoani Morogoro kwenda Zanzibar kupata elimu na ujuzi wa uzalishaji wa mazao hayo.

“...nitoe wito  tuendelee kuungana, kushirikiana kubadilishana wataalam, kufanya vikao vya pamoja ili kuhakikisha mazao haya yanakuwa na tija ya uzalishaji..” amesema Mhe. Shamata Shaame Khamis.

Waziri wa kilimo, umwagiliaji, maliasili na Mifugo Mhe. Shamata Shaame Khamis (wa pili kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Morogoro Bi. Joanfaith Kataraia baada ya kutembelea banda la Halmashauri hiyo.

Sambamba na hilo, Mhe. Shamata wakati akiwa kwenye banda la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) amesisitiza watendaji wa mamlaka hiyo kufanya kazi kwa weledi na kwa ushirikiano ili kutimiza lengo la serikali katika ukusanyaji wa mapato.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima amemshukuru Waziri huyo kwa kutembelea maonesho hayo Kanda ya Mashariki na kukubali kupokea wataalam ambao watapata uzoefu juu ya uzalishaji wa mazao ya kimkakati hususan zao la karafuu.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam (katikati) Malima akiwa amemshika samaki aina ya ngulu wanaopatikana katika banda la Halmashauri ya Mafia.

Mhe. Malima ameongeza kuwa itaundwa timu ya wataalam 30 wakiwemo wakulima 20, maafisa kilimo 5, waandishi wa habari 5 ambao wataenda kujifunza namna bora ya uzalishaji wa karafuu, aidha, amesema ziara ya Waziri huyo itafungua fursa za kilimo kwa wakulima wa Kanda ya Mashariki.

Kwa niaba ya waoneshaji, Bw. Abdalah Mkazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ambaye ana ulemavu wa macho amesema maonesho ya Nanenane 2023 hayajawaacha nyuma watu wenye ulemavu ambapo imetoa fursa kwao kuonesha ujuzi walionao, hivyo ameishukuru Serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia nafasi hiyo. Ameongeza kuwa amebuni kifaa cha kuingiza uzi kwenye sindano kitakacho wasaidia mafundi wasioona kushona nguo.

Pichani ni Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akisalimiana na viongozi mbalimbali.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.