Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amefuta mashamba pori 11 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro yenye ukubwa wa ekari 24,119 na kuyarejesha kwa wananchi kwaajili ya kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kilimo na ufugaji.
Hayo yamebainishwa Juni 7, mwaka huu na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi (Mb) wakati wa ziara yake ya siku mojaWilayani humo iliyolenga kurejesha mashamba kwa wananchi yaliyobatilishwa na Serikali baada ya kuona hayaendelezwi.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.