ZIARA YAKIKAZI YA WAZIRI WA UJENZI MOROGORO
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashugwa amewasili Mkoani Morogoro leo Februari 21, 2024 kwa ziara ya kikazi ya siku nne kwa ajili ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mkoani humo miradi ya Sekta ya miundombinu hususan barabara.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo
Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Ali Malima akiwa na mgeni wake Waziri wa Ujenzi
Akiwa Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa huo kusaini kitabu cha wageni, ameongea mbele ya waandishi wa Habari kuwa ziara hiyo ni utekelezaji wa moja ya maagizo ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuwataka viongozi wa serikali kufika maeneo yasiyo fikika ili kutatua changamoto za miundombinu ya barabara.
Aidha amesema Mkoa wa Morogoro, una mchango mkubwa kwa uzalishaji wa chakula hapa nchini, na amesema kwa vile Mkoa wa Morogoro ni Mkoa wa Kimkakati kwenye kilimo maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuboresha miundombionu ya Barabara na kuunganisha na mikoa au maeneo mengine.
kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema pamoja na ziara ya Mhe. Waziri wa Ujenzi kuwa na ziara ya maeneo mbalimbali ya Mkoa huo kukagua miundombinu ya barabara, Mhe. Malima amewasilisha ombi maalum kwa Waziri huyo, ya kupeleka Box Calvati kwa ajili ya kuboresha barabara ya Ifakara - Mlimba ambayo inayokabiliwa na madaraja mengi kutokana na kuwa na mito midogomidogo mingi na kusababisha changamoto kubwa ya barabara hiyo kutopitika hususan wakati wa masika.
Mhe. Waziri Bashungwa anatarajia kuanza rasmi ziara yake hapo kesho Februari 22, 2024 na kutembelea Halmashauri za Kilosa, Gairo, Ifakara, Mlimba na Morogoro DC. Kwa lengo la kukagua miundombinu ya Barabara.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.