Msajili wa Vyama vya siasa nchini Jaji Francis Mutungi amewataka wajumbe wa Baraza la vyavya vya siasa hapa nchini kuhakikisha wanazingatia Sheria za nchi, Kanuni na Katiba za vyama vyao katika utendaji kazi wao ili kuepuka migogoro na migongano ya kisiasa ambayo husababisha uwepo wa hali mbaya ya kisiasa nchini.
Jaji Mutungi ametoa wito huo Leo Mei 14, wakati akifungua kikao cha kawaida cha Baraza la Vyama vya Siasa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Nashera uliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Kiongozi huyo amesema wanachama wa vyama vya siasa wanawajibu wa kuzingatia sheria za nchi kanuni na katiba za vyama vyao ili kuhakikisha wanafanya yaliyo sahihi ili kuondokana na migogoro ndani ya vyama na kuhakikisha maendeleo yanafanyika ndani ya chama na nje ya chama.
".. Nawasihi mzingatie Sheria za nchi, mzingatie katiba za vyama vyenu na sheria zinazosimamiwa na Baraza la vyama vya siasa.." ameisisitiza Jaji Francis Mutungi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Dkt. Emmanuel Lameck ametoa wito kwa vyama vyote vya siasa visajiliwe kwenye Tume hiyo ili kuwezesha kuweka usiri wa faragha ya mtu jambo ambalo litaenda kuongeza imani kwa watu ndani ya vyama vya siasa kwa maslahi ya mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Civic United Front (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba ameishukuru tume hiyo kwa kuja na mafunzo hayo ambayo yataenda kuhakikisha faragha za wanachama wa vyama mbalimbli zinabadi kuwa siri pia kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ni jukumu la vyama vya siasa kubadilika na kuhakikisha taarifa binafsi za kila mwananchama zinatunzwa na kuwa siri ili zisitumike vibaya.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.