Taarifa ya Miradi ya Maendeleo Julai 2021 hadi Juni 2022 Morogoro
UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO JULAI 2021 HADI JUNI 2022 MKOA WA MOROGORO
1. MAPITIO YA BAJETI YA SEKRETARIETI YA MKOA NA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA 2021/2022
Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Mkoa wa Morogoro uliidhinishiwa jumla ya Shilingi 399,349,347,617/= kwa ajili ya kutekeleza kazi za Serikali kwa Sekretarieti ya Mkoa na Halmashauri 9 kwa mchanganuo ufuatao: -
i. Mishahara shilingi 249,552,832,594/=.
Kiasi kilichopokelewa hadi Juni 2022 ni shilingi 249,552,832,594/= sawa na asilimia 100, Matumizi kwa kipindi hicho yalifikia shilingi 249,552,832,594/= sawa na asilimia 100
ii. Matumizi Mengineyo shilingi 16,279,468,361/=
Kiasi kilichopokelewa hadi Juni 2022 ni shilingi 16,279,468,361/= sawa na asilimia 100, Matumizi kwa kipindi hicho yalifikia shilingi 16,279,468,361/= swa na asilimia 100.
iii. Fedha za Maendeleo shilingi 93,320,850,350/=.
Fedha za Ndani zikiwa ni shilingi 42,792,834,350/= na Fedha za Nje shilingi 50,528,016,000/=
Kiasi cha Fedha kilichopokelewa hadi mwezi Juni 2022 kilikuwa shilingi 121,610,850,350/= sawa na asilimia 130 ya fedha zilizoidhinishwa.
Fedha zilizopokelewa Nje ya Bajeti iliyoidhinishwa ni shilingi 33,930,000,000/= za ujenzi wa Miundombinu ya Sekta ya Afya na Elimu kwa mchanganuo ufuatao.
2
Na.
Mradi la Mradi
i
UVIKO Elimu
shilingi
17,220,000,000
ii.
UVIKO Afya
shilingi
4,270,000,000
iii
Tozo – Afya
shilingi
5,500,000,000
iv
Tozo Elimu
shilingi
900,000,000
v
LANES
shilingi
400,000,000
SEQUIP
shilingi
5,640,000,000
Jumla
shilingi
33,930,000,000
2. MIRADI YA SEKTA YA ELIMU
Mkoa wa Morogoro kwa mwaka 2021/22 ulidhinishiwa Shilingi 26,105,038,350/= kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Elimu Msingi na Sekondari. Hadi Juni 2022 Mkoa ulikuwa umepokea shilingi 50,025,038,350/= sawa na asilimia 193 ya Fedha zilizoidhinishwa na Bunge kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi ya Elimu. Ongezeko la shilingi 24,160,000,000/= sawa na asilimia 92.5 ya bajeti iliyoidhinishwa kwa sekta ya elimu zilielekezwa kwenye ujenzi wa vyumba 707 vya madarasa katika shule za Sekondari, Ujenzi wa vyumba 142 vya madarasa Shule za Msingi (Shikizi) chini ya Programu ya Uviko. Ujenzi wa shule ya Msingi Tambukareli Kilosa chini ya Programu ya LANES, Ujenzi wa shule za Sekondari 12 mpya chini ya Programu ya SEQUIP na Ukamilishaji wa vyumba 35 vya madarasa chini ya Fedha za Tozo za Miamala ya simu.
3
Mchanganuo wa fedha za Miradi ya Elimu zilizopokelewa na kazi zilizofanyika ni kama ifuatavyo:
Jedwali Na. 1:Miradi ya Sekta ya Elimu mwaka 2021/2022
Na.
Kazi
Idadi
Shilingi
Ukamilishaji
1.
Ukamilishji wa vyumba vya madarasa shule za Msingi
96
1,199,610,350
100%
2.
Ukamilishaji wa vyumba ya madarasa shule za Sekondari
96
1,200,000,000
100%
3.
Ukamilishaji wa Maabara za Sayansi shule za Sekondari
46
1,425,000,000
100%
4.
Elimu Msingi bila malipo kwa shule za msingi
7,256,880,000
100%
5.
Elimu bila malipo kwa shule za Sekondari
7,839,195,000
100%
6.
Fedha za Mitihani kwa shule za Msingi na Sekondari
6,694,579,000
100%
7.
Usimamizi wa mitihani kwa shule za Msingi na Serikali
209,774,000
100%
8.
Ukamilishaji wa Bweni 1 Shule ya Sekondari Kipingu
1
40,000,000
90%
Jumla Ndodo
25,865,038,350
9. Ukamilishaji wa vyumba vya madarasa (TOZO) 35 900,000,000 90%
10 Ujenzi wa shule ya Msingi Tambukareli Kilosa (LANES) 1 400,000,000 80%
11 Ujenzi wa shule mpya za Sekondari (SEQUIP) 12 5,640,000,000 80%
MIRADI YA UVIKO
12. Ujenzi wa Bweni shule za Msingi 3 240,000,000 60%
13 Ujenzi wa vyumba vya madarasa Sekondari 707 14,140,000,000 100%
14 Ujenzi wa vyumba vya madarasa Shule za Msingi (Shikizi) 142 2,840,000,000 100%
Jumla ya Miradi ya UVIKO
17,220,000,000
Jumla Sekta ya Elimu
50,025,038,350
4
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.